Saturday, May 28, 2016

Mafanikio tuliyopata

Fslh dlashd kjsah dsah dksa hdkjsa hdksaas dhjksa
Tuieleza kuwa Serikali ya George W. Bush ilifanya mpango ili watu wa ukoo wa Osama bin Laden waondolewe Marekani ili wasibughudhiwe. Machi 28, 2005, gazeti ‘Daily Time’s la Pakistan, likiripoti kutoka Washington DC., Marekani, lilidai kuwa FBI (Shirika la Upelelezi la Marekani) iliwasaidia Wasaudia kuondoka baada ya mashambulizi ya Septemba 11.”

Mtangazaji wa BBC, Greg Palast, alisema kipindi cha ‘Newsnight’ cha BBC kimegundua historia ndefu ya “uhusiano wa karibu sana” ulioko kati ya Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA), Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na Wasaudia. (rejea http://goo.gl/NDCQmJ).

Michael Springman ambaye alikuwa kwenye dawati la kutoa visa mjini Jeddah, Saudi Arabia, kuanzia mwaka 1987 hadi 1989, alikaririwa na ‘BBC Newsnight’ akisema: “Nchini Saudi Arabia nilikuwa nikilazimishwa na maofisa wa ngazi za juu wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje (ya Marekani) nitoe visa kwa waombaji ambao hawakuwa na sifa ya kuzipata.

“Wengi wa hawa ni wale ambao hawakuwa na uhusiano na Saudi Arabia au Marekani. Nililalamika sana mjini Jeddah. Nilirudi hata Marekani kuilalamikia ofisi ya Mambo ya Nje … lakini sikusikilizwa … Nilichokuwa napinga kwa kweli ni kuingiza nchini (Marekani) askari wapya wa Osama bin Laden. Waliingiza nchini Marekani kufundishwa na CIA, ambao baada ya mafunzo walikuwa wakipelekwa Afghanistan ili kupigana dhidi ya Urusi.”

Upo hapo? Tilia mkazo maneno ya Springman: “ …askari wapya wa Osama bin Laden waliingiza nchini Marekani kufundishwa na CIA…”

Kauli ya Springman aliitoa wakati ule ambao Urusi ilikuwa imeikalia Afghanistan na vita yao dhidi ya Urusi ambayo ilikuwa ikipiganwa na mujahidina, akiwamo Osama bin Laden, ikawa inasimamiwa na CIA.

Wakati Springman akitoa madai hayo ulikuwa ni kati ya mwaka 1987 na 1989, au 1990. Huo ndio wakati ule ambao George H. Bush, ambaye awali alikuwa mkurugenzi wa CIA, alipoingia madarakani kuwa Rais wa 41 wa Marekani.
banner
Habari ya Nyuma
Habari Mpya

0 comments: