![]() |
| Tilia mkazo maneno ya Springman |
Upo hapo? Tilia mkazo maneno ya Springman: “ …askari wapya wa Osama bin Laden waliingiza nchini Marekani kufundishwa na CIA…”
Kauli ya Springman aliitoa wakati ule ambao Urusi ilikuwa imeikalia Afghanistan na vita yao dhidi ya Urusi ambayo ilikuwa ikipiganwa na mujahidina, akiwamo Osama bin Laden, ikawa inasimamiwa na CIA.
Wakati Springman akitoa madai hayo ulikuwa ni kati ya mwaka 1987 na 1989, au 1990. Huo ndio wakati ule ambao George H. Bush, ambaye awali alikuwa mkurugenzi wa CIA, alipoingia madarakani kuwa Rais wa 41 wa Marekani.
Mtangazaji wa BBC, Greg Palast, alisema kipindi cha ‘Newsnight’ cha BBC kimegundua historia ndefu ya “uhusiano wa karibu sana” ulioko kati ya Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA), Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na Wasaudia. (rejea http://goo.gl/NDCQmJ).
Michael Springman ambaye alikuwa kwenye dawati la kutoa visa mjini Jeddah, Saudi Arabia, kuanzia mwaka 1987 hadi 1989, alikaririwa na ‘BBC Newsnight’ akisema: “Nchini Saudi Arabia nilikuwa nikilazimishwa na maofisa wa ngazi za juu wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje (ya Marekani) nitoe visa kwa waombaji ambao hawakuwa na sifa ya kuzipata.


0 comments: