![]() |
| U hdajl hdsakjhd kjashd ksa dhjksah djksa |
“Wengi wa hawa ni wale ambao hawakuwa na uhusiano na Saudi Arabia au Marekani. Nililalamika sana mjini Jeddah. Nilirudi hata Marekani kuilalamikia ofisi ya Mambo ya Nje … lakini sikusikilizwa … Nilichokuwa napinga kwa kweli ni kuingiza nchini (Marekani) askari wapya wa Osama bin Laden. Waliingiza nchini Marekani kufundishwa na CIA, ambao baada ya mafunzo walikuwa wakipelekwa Afghanistan ili kupigana dhidi ya Urusi.”
Upo hapo? Tilia mkazo maneno ya Springman: “ …askari wapya wa Osama bin Laden waliingiza nchini Marekani kufundishwa na CIA…”
Kauli ya Springman aliitoa wakati ule ambao Urusi ilikuwa imeikalia Afghanistan na vita yao dhidi ya Urusi ambayo ilikuwa ikipiganwa na mujahidina, akiwamo Osama bin Laden, ikawa inasimamiwa na CIA.
Wakati Springman akitoa madai hayo ulikuwa ni kati ya mwaka 1987 na 1989, au 1990. Huo ndio wakati ule ambao George H. Bush, ambaye awali alikuwa mkurugenzi wa CIA, alipoingia madarakani kuwa Rais wa 41 wa Marekani.


0 comments: