Yote hayo yalidaiwa kuwa aliyeyafanya ni Osama, lakini uchunguzi dhidi yake unakwamishwa. Isitoshe, Minara ya Khobar iliyolipuliwa kwa bomu Jumatano ya Juni 25, 1996 katika eneo la majengo ya kambi ya kijeshi eneo la Dhahran, Saudi Arabia, ilidaiwa kuwa aliyetekeleza ugaidi huo ni Osama, lakini cha ajabu ni kwamba familia ya Bin Laden ndiyo iliyopewa kazi ya kujenga upya majengo ya minara hiyo.
‘Newsnight’ ilisema baada ya George W. Bush kuwa Rais wa Marekani, FBI waliambiwa waache kuichunguza familia hiyo ya Kisaudia. Greg Palast anasema siku chache baada ya Septemba 11, na wakati ‘washukiwa’ wa Kiislamu na wengine wote wenye asili au sura za Kiarabu wakiwa wanazingirwa kila mahali nchini Marekani, ndege maalumu ilitolewa ambayo iliwasafirisha watu 11 wa familia ya Bin Laden kutoka Marekani na kuwapeleka Saudi Arabia.
Watu hao walipanda ndege kutoka kwenye uwanja ule ule wa Boston ambamo ndege iliyoshambulia WTC iliondokea. Na bado dunia inaambiwa kuwa Osama ni gaidi aliyekuwa akitafutwa sana na Marekani?
Pengine wangebadilisha kauli kwa mujibu wa taarifa zilizotajwa hapo juu. Badala ya kusema Osama ni gaidi aliyekuwa akitafutwa sana na Marekani, waseme Osama ni gaidi aliyelindwa sana na Marekani.
Wengi wana mengi ya kusema juu ya jambo hili. Jean-Charles Brisard ni Mfaransa ambaye ni mtaalamu na mshauri wa kimataifa kuhusu ugaidi. Aliwahi kuandika kitabu kuhusu mtandao wa fedha wa familia ya Bin Laden.
Kitabu hicho alikiita ‘The Economic Environment of Osama Bin Laden’. Brisard aliheshimiwa sana na Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, kutokana na kazi zake, hususan kazi za utafiti. Brisard anasema mwaka 1998 Osama aliweza kutumia fedha na mawasiliano yote aliyoweza kuyapata nchini Saudi Arabia na alikuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na maofisa kadhaa wa Serikali ya Saudi Arabia.
Isitoshe, anasema Brisard, Serikali ya Saudi Arabia ilikuwa ikiwasaidia Taliban ambao wanadaiwa kuwa walikuwa wakimhifadhi Osama nchini Afghanistan. “Katika nchi ya Saudi Arabia, mkono wa kushoto hupuuza mkono wa kulia,” anaandika Brisard na kuongeza, “…na FBI walijua fika hali halisi ya mambo.”
Brisard na mtu mwingine, Guillaume Dasquie, ambaye ni mwandishi wa habari wa Ufaransa aliyebobea katika habari za ugaidi, waliandika kitabu wanachokiita ‘Bin Laden: The Forbidden Truth’, ambacho chapa yake ya awali ni ya Kifaransa.
Ukuta wa Berlin na usafi wake
on 7:03:00 AM

Hii ni kali sana. Naipongeza Way Cleaners
ReplyDeleteUbarikiwe sana
ReplyDelete